|
Post by Admin on Feb 27, 2016 10:03:14 GMT
Kampuni ya Apple imeitaka mahakama moja ya Marekani kubatilisha uamuzi wake wa hapo awali ulioiagiza kampuni hiyo kulisaidia shirika la kijasusi la FBI kuifungua simu yake iliotumika na muuaji wa eneo la San Bernardino. Katika nakala zake za mahakamani, Apple imesema kuwa watekelezaji sheria wanatafuta uwezo hatari na hatua hiyo inakiuka haki za kikatiba. Shirika la FBI na ikulu ya Whitehouse zimesema ombi hilo ni la kuifungua simu moja pekee. Lakini Apple inasema kuwa programu inayohitajika ili kutimiza ombi la FBI haipo. Badala yake Apple inasema italazimika kutengeza toleo jipya la programu ya simu hiyo itakayofunguliwa kupitia mlango wa nyuma ili kuweza kupata data hiyo. Imehoji kwamba mahakama hiyo haina uwezo wa kuilazimisha Apple kufanya hivyo. Apple pia imesema kuwa hakuna mahakama ambayo imeilazimisha kampuni yoyote kupunguza usalama wa bidhaa zake ili kuweza kuingia na kuchukua habari ya mtu binafsi. ''Kesi hii ni kuhusu idara ya haki na FBI inatafuta nguvu zenye hatari ambazo bunge na raia wa Marekani wamezihifadhi,''ombi hilo lilisema.
|
|