|
Post by Admin on Feb 27, 2016 10:09:31 GMT
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Apple Tim Cook, amewalaumu wachunguzi wa shirika la ujasusi nchini Marekani FBI kwa vile walivyokubali kuisaidia mahakama kuifungua simu ya aina ya iphone ya Syed Rizwan Farook wa eneo la San Bernardino. Bwana Cook amekiambia kituo cha runinga cha ABC kwamba kampuni yake iligundua ombi hilo la kutatanisha katika vyombo vya habari. ''sidhani hiyo ndio njia nzuri ya kufanya kazi ,alisema.''sidhani kitu cha muhimu kwa nchi hii hutatuliwa kama hivyo.'' Hata hivyo, mtu wa karibu wa uchunguzi huo ameiambia BBC Bwana Cook anadai ''kwa ufupi haikuwa ukweli ''na kuwa timu ya kisheria ya Apple ilikuwa ya 'kwanza kugundua' Msemaji wa wachunguzi wa shirika la ujasusi la FBI , amesema hangetaka kusema lolote kuhusiana na matamshi ya Bwana Cook. Kwengineko, gazeti la New York Times limeripoti kwamba Apple imeanza kuimarisha vifaa vyake, ambavyo vitaimarisha simu za Apple na kuzifanya kuwa vigumu kuifungua simu ya iPhone kutumia njia iliyowasilishwa na shirika la FBI katika kesi hiyo.
|
|